The chat will start when you send the first message.
1Ikawa baada ya kufa kwake Sauli, hapo Daudi aliporudi katika kuwaua Waamaleki, naye Daudi amekaa siku mbili katika Siklagi;[#1 Sam 11:11; 30:17,26; 1 Fal 20:29,30]
2hata siku ya tatu ikawa, tazama! Akaja mtu kutoka kambi ya Sauli, nguo zake zimeraruliwa, tena ana mavumbi kichwani mwake; basi, ikawa alipomfikia Daudi, akaanguka chini, akamsujudia.[#2 Sam 4:10; Mwa 37:29; 44:13; Hes 14:6; Yos 7:6; 1 Sam 4:12; Ayu 1:20; Mdo 14:14]
3Daudi akamwambia, Umetoka wapi? Akamwambia, Nimeokoka katika kambi ya Israeli.
4Daudi akamwambia, Mambo yalikuwaje? Tafadhali niambie. Akajibu, Watu wamekimbia vitani, tena watu wengi wameanguka wamekufa; hata Sauli naye na Yonathani, mwanawe, wamekufa.[#1 Sam 4:16]
5Daudi akamwambia yule kijana aliyempa habari, Umejuaje ya kuwa Sauli na Yonathani mwanawe wamekufa?
6Yule kijana aliyempa habari akasema, Nilikuwapo kwa nasibu juu ya kilima cha Gilboa, na tazama, Sauli alikuwa ameegemea fumo lake; na tazama, magari na wapanda farasi wanamfuatia kwa kasi.[#1 Sam 31:1-6; 1 Nya 10:1-6]
7Naye alipotazama nyuma, akaniona, akaniita. Nikajibu, Mimi hapa.
8Akaniambia, U nani wewe? Nikamjibu, Mimi ni Mwamaleki.
9Akaniambia, Tafadhali simama karibu nami, ukaniue, maana shida imenipata; kwa sababu roho yangu ingali hai ndani yangu.
10Basi, nikasimama karibu naye, nikamwua, kwa sababu nilijua hakika ya kuwa hawezi kupona baada ya kuanguka; kisha nikalitwaa lile taji lililokuwa kichwani mwake, na kikuku kilichokuwa mkononi mwake, nami nimevileta hapa kwa bwana wangu.[#Amu 9:54]
11Ndipo Daudi akashika nguo zake akazirarua na kadhalika watu wote waliokuwa pamoja naye;[#Yos 7:6; 2 Sam 3:31; 13:31; 2 Nya 34:27; Ezr 9:3; Yoe 2:13]
12wakaomboleza, wakalia, wakafunga hadi jioni, kwa ajili ya Sauli, na kwa ajili ya Yonathani mwanawe, na kwa ajili ya watu wa BWANA na kwa ajili ya nyumba ya Israeli; kwa sababu wameanguka kwa upanga.
13Naye Daudi akamwambia yule kijana aliyempa habari, Unatoka wapi wewe? Akajibu, Mimi ni mwana wa mgeni, Mwamaleki.
14Daudi akamwambia, Jinsi gani hukuogopa kuunyosha mkono wako umwangamize masihi wa BWANA?[#Hes 12:8; 1 Sam 24:6; Zab 105:15; #1:14,16 Au, mtiwa mafuta (tazama 1 Sam 2:10).]
15Ndipo Daudi akamwita mmoja wa vijana, akamwambia, Mwendee, ukamwangukie. Basi akampiga hadi akafa.[#Amu 8:20; 1 Sam 22:17,18; 2 Sam 4:10; 1 Fal 2:25,34,46]
16Daudi akamwambia, Damu yako na iwe juu ya kichwa chako mwenyewe; maana umejishuhudia nafsi yako ukisema, Nimemwua masihi wa BWANA.[#1 Sam 26:9; 1 Fal 2:32; Lk 19:22; #1:14,16 Au, mtiwa mafuta (tazama 1 Sam 2:10).]
17Basi Daudi akamwomboleza Sauli, na Yonathani, mwanawe, maombolezo haya;
18(kama ilivyoandikwa katika kitabu cha Yashari), akasema,[#Yos 10:13]
Wana wa Yuda na wafundishwe haya,
19Walio fahari yako, Ee Israeli
Juu ya mahali pako palipoinuka wameuawa;
Jinsi mashujaa walivyoanguka!
20Msiyahubiri mambo haya katika Gathi,[#Amu 16:23; 1 Sam 31:9; Mik 1:10; Kut 15:20; Amu 11:34; 1 Sam 18:6; 31:4]
Msiyatangaze katika njia za Ashkeloni;
Wasije wakashangilia binti za Wafilisti,
Binti za wasiotahiriwa wakasimanga.
21Enyi milima ya Gilboa, visiwepo juu yenu[#Amu 5:23; Ayu 3:3,4; Yer 20:14; 1 Sam 10:1]
Umande wala mvua, wala mashamba ya matoleo;
Maana ndipo ilipotupwa kwa aibu ngao ya shujaa,
Ngao yake Sauli, pasipo kutiwa mafuta.
22Kutoka kwa damu yao waliouawa,[#1 Sam 18:4]
Kutoka kwa shahamu yao mashujaa,
Upinde wa Yonathani haukurudi nyuma,
Wala upanga wa Sauli haukurudi bure.
23Sauli na Yonathani walipendwa na kupendeza[#Amu 14:18]
Maishani wala mautini hawakutengwa;
Walikuwa wepesi kuliko tai,
Walikuwa hodari kuliko simba.
24Enyi binti za Israeli, mlilieni
Huyo Sauli, ambaye aliwavika
Mavazi mekundu kwa anasa,
Akazipamba nguo zenu dhahabu.
25Jinsi mashujaa walivyoanguka
Katikati ya vita!
Ee Yonathani, wewe umeuawa
Juu ya mahali pako palipoinuka.
26Nimesikitika kwa ajili yako, Yonathani, ndugu yangu,[#1 Sam 18:1,3; 19:2; 20:17]
Ulikuwa ukinipendeza sana;
Upendo wako kwangu ulikuwa wa ajabu,
Kupita upendo wa wanawake.
27Jinsi mashujaa walivyoanguka,
Na silaha za vita zilivyoangamia!