The chat will start when you send the first message.
1Ninyi akina bwana, wapeni watumishi wenu yaliyo haki na ya adili, mkijua ya kuwa ninyi nanyi mna Bwana mbinguni.[#Efe 6:9; Law 25:43,53]
2Dumuni sana katika kuomba, mkikesha katika kuomba mkiwa na shukrani;[#1 The 5:17; Efe 6:18; Flp 4:6]
3mkituombea na sisi pia, kwamba Mungu atufungulie mlango kwa lile neno lake, tuinene siri ya Kristo, ambayo kwa ajili yake nimefungwa,[#Rum 15:30; Efe 6:18,19; 2 The 3:1; 1 Kor 16:9]
4ili niidhihirishe, kama inipasavyo kunena.[#Efe 6:20]
5Nendeni kwa hekima mbele yao walio nje, mkiukomboa wakati.[#Efe 5:15,16; 1 The 4:12]
6Maneno yenu yawe na neema siku zote, yakikolezwa chumvi, ili mpate kujua jinsi iwapasavyo kumjibu kila mtu.[#Efe 4:29; Mk 9:50; 1 Pet 3:15]
7Tikiko, ndugu mpendwa, mtumishi mwaminifu, mwenzi wangu katika Bwana, atawaarifu mambo yangu yote;[#Mdo 20:4; 2 Tim 4:12; Efe 6:21]
8ambaye nimemtuma kwenu kwa sababu iyo hiyo, ili mjue mambo yetu, naye akawafariji mioyo yenu;[#Efe 6:22]
9pamoja na Onesimo, ndugu mwaminifu, mpendwa, aliye mtu wa kwenu. Hao watawaarifu mambo yote ya hapa petu.[#Flm 1:10-12]
10Aristarko, aliyefungwa pamoja nami, awasalimu; pamoja na Marko, binamu yake Barnaba, ambaye mmepokea maagizo juu yake; akifika kwenu mkaribisheni.[#Mdo 12:12,25; 13:13; 15:37-39; 18:27; 19:29; 27:2; Flm 1:24]
11Na Yesu aitwaye Yusto awasalimu. Hao tu ndio watu wa tohara miongoni mwa wale watendao kazi pamoja nami kwa ajili ya ufalme wa Mungu; nao wamekuwa msaada kwangu.[#4:11 Katika makala zingine ni Yoshua.]
12Epafra, aliye mtu wa kwenu, mtumwa wa Yesu Kristo, awasalimu, akifanya bidii siku zote kwa ajili yenu katika maombi yake, ili msimame mkiwa wakamilifu na kuthibitika kabisa katika mapenzi yote ya Mungu.[#Kol 1:7; Flm 1:23]
13Maana namshuhudia kwamba ana juhudi nyingi kwa ajili yenu, na kwa ajili ya hao walioko Laodikia, na kwa ajili ya hao walioko Hierapoli.
14Luka, yule tabibu mpendwa, na Dema, wanawasalimu.[#2 Tim 4:10,11; Flm 1:24]
15Wasalimuni ndugu walioko Laodikia, na Nimfa, na kanisa lililo katika nyumba yake.
16Waraka huu ukiisha kusomwa kwenu hakikisheni kwamba unasomwa katika kanisa la Walaodikia pia; na ule wa Laodikia usomwe na ninyi.
17Mwambieni Arkipo, Iangalie sana huduma ile uliyopewa katika Bwana, ili uitimize.[#Flm 1:2]
18Naandika salamu yangu mimi Paulo, kwa mkono wangu mwenyewe. Kumbukeni kufungwa kwangu. Neema na iwe pamoja nanyi.[#1 Kor 16:21; 2 The 3:17]