The chat will start when you send the first message.
1BWANA akanena na Musa, na kumwambia,
2Siku ya kwanza ya mwezi wa kwanza utaisimamisha hiyo maskani ya hema ya kukutania.[#Kut 12:2; 13:4; 25:9; 26:1,30; Hes 7:1; Mdo 7:44,45; Ebr 8:2-5; 9:2,11; Ufu 21:3]
3Nawe utatia ndani yake sanduku la ushuhuda, nawe utalisitiri hilo sanduku kwa pazia.[#Hes 4:5]
4Nawe utaleta meza na kuitia ndani, na kuviweka sawasawa vile vitu juu yake; kisha utakileta ndani kile kinara cha taa, na kuziwasha taa zake.[#Kut 26:35; Law 24:5,6]
5Kisha utaisimamisha madhabahu ya dhahabu kwa kufukizia uvumba mbele ya sanduku la ushuhuda, na kulitia pazia mlangoni mwa hiyo maskani.[#Ebr 9:24; 10:19-22]
6Kisha utaweka madhabahu ya kuteketeza sadaka mbele ya mlango wa maskani ya hema ya kukutania.
7Kisha utaliweka birika kati ya hema ya kukutania na hiyo madhabahu, nawe utatia maji ndani yake.[#Kut 30:18]
8Kisha utausimamisha ukuta wa ua kuuzunguka pande zote, na kuitundika sitara ya lango la ua.
9Kisha utayatwaa mafuta ya kutiwa, na kuitia mafuta hiyo maskani, na kila kitu kilicho ndani yake, na kuiweka iwe takatifu, na vyombo vyake vyote; nayo itakuwa takatifu.[#Kut 30:23-26]
10Kisha utaitia mafuta madhabahu ya kuteketeza sadaka, na vyombo vyake vyote; na kuiweka takatifu madhabahu; na hiyo madhabahu itakuwa takatifu sana.[#Kut 29:36]
11Kisha utalitia mafuta birika na kitako chake, na kuliweka liwe takatifu.
12Kisha utamleta Haruni na wanawe hapo mlangoni pa hema ya kukutania, nawe utawaosha kwa maji.[#Law 8:1-13]
13Kisha utamvika Haruni mavazi matakatifu; nawe utamtia mafuta, na kumweka awe mtakatifu, ili apate kunitumikia katika kazi ya ukuhani.[#Kut 28:41; Zab 133:2]
14Kisha utawaleta wanawe, na kuwavika kanzu zao;[#Ebr 7:23]
15nawe utawatia mafuta kama ulivyomtia mafuta baba yao, ili wanitumikie katika kazi ya ukuhani; na huko kutiwa mafuta kwao kutakuwa ni kwa ukuhani wa milele katika vizazi vyao vyote.[#Hes 25:13; Ebr 7:11; Ufu 1:6; 1 Pet 2:5,9]
16Musa akafanya hayo yote; kama BWANA aliyoagiza ndivyo alivyofanya yote.
17Hata mwezi wa kwanza wa mwaka wa pili, siku ya kwanza ya mwezi maskani ile ilisimamishwa.[#Hes 7:1]
18Musa akaisimamisha maskani, akaviweka vitako vyake, akazisimamisha mbao zake akayatia mataruma yake, akazisimamisha nguzo zake.
19Akaitanda hema juu ya maskani, akakitia kifuniko cha hema juu yake; kama BWANA alivyomwamuru Musa.
20Akautwaa ule ushuhuda, akautia ndani ya sanduku, akaiweka miti ya kuchukulia juu ya sanduku, akakiweka kiti cha rehema juu ya sanduku;[#Kut 25:16; Zab 78:5; Isa 8:20]
21kisha akalileta sanduku akalitia ndani ya maskani, naye akalitundika pazia la sitara, akalisitiri sanduku la ushuhuda; kama BWANA alivyomwamuru Musa.[#Kut 35:12]
22Akaitia meza ndani ya hema ya kukutania, upande wa maskani ulioelekea kaskazini, nje ya pazia.[#Kut 26:35]
23Akaipanga ile mikate juu yake mbele za BWANA; kama BWANA alivyomwamuru Musa.
24Kisha akakitia kinara cha taa ndani ya hema ya kukutania, kuikabili ile meza, upande wa maskani ulioelekea kusini.[#Kut 26:35]
25Kisha akaziwasha taa zake mbele za BWANA, kama BWANA alivyomwamuru Musa.[#Kut 25:37]
26Akaitia madhabahu ya dhahabu ndani ya hema ya kukutania mbele ya pazia.[#Kut 30:6]
27Akafukiza juu yake uvumba wa manukato kama BWANA alivyomwamuru Musa.[#Kut 30:7]
28Akalitia pazia la mlango wa maskani.[#Kut 26:36]
29Akaiweka madhabahu ya sadaka ya kuteketezwa mlangoni pa maskani ya kukutania, akatoa sadaka ya kuteketezwa juu yake, na sadaka ya unga; kama BWANA alivyomwamuru Musa.[#Kut 29:38]
30Akaliweka birika kati ya hema ya kukutania na madhabahu, akatia maji ndani yake ya kuoshea.[#Kut 30:18]
31Musa na Haruni, na wanawe wakanawa mikono yao na miguu yao ndani yake;
32hapo walipoingia hema ya kukutania, na hapo walipoikaribia madhabahu walinawa kama BWANA alivyomwamuru Musa.[#Kut 30:19]
33Akausimamisha ukuta wa ua kuizunguka maskani na madhabahu, akalitundika pazia la mlango wa ule ua. Basi Musa akaimaliza hiyo kazi.[#Kut 27:9,16]
34Ndipo lile wingu likaifunikiza hema ya kukutania, na huo utukufu wa BWANA ukaijaza maskani.[#1 Fal 8:10-11; Isa 6:4; Eze 43:4-5; Ufu 15:8; Law 16:2; Hes 9:15; 2 Nya 5:13; 7:2; Hag 2:7,9]
35Wala Musa hakuweza kuliingia hema la kukutania, kwa sababu lile wingu lilikaa juu yake, na huo utukufu wa BWANA ukaijaza maskani.[#1 Fal 8:11; 2 Nya 5:14; Zab 78:14]
36Na hapo lile wingu lilipoinuliwa kutoka juu ya maskani, wana wa Israeli wakaenda mbele katika safari zao zote,[#Hes 10:11; Neh 9:19]
37bali kama lile wingu halikuinuliwa, wakati ule hawakusafiri hadi siku ile lilipoinuliwa tena.[#Hes 9:19-22]
38Kwa maana lile wingu la BWANA lilikuwa juu ya maskani wakati wa mchana, na mlikuwa na moto ndani yake wakati wa usiku, mbele ya macho ya nyumba ya Israeli katika safari zao zote.[#Kut 13:21; Hes 9:15]