The chat will start when you send the first message.
1Ndipo Ayubu akajibu, na kusema,
2Nimesikia maneno mengi mfano wa hayo;
Ninyi nyote ni wafariji wenye kutaabisha.
3Je! Maneno yasiyo faida yatakuwa na mwisho?
Au, kuna nini kinachokukasirisha, hata ukajibu?
4Mimi nami ningeweza kunena kama ninyi;[#2 Fal 19:21; Zab 22:7; Yer 18:16; Omb 2:15]
Kama roho zenu zingekuwa mahali pa roho yangu,
Ningeweza kutunga maneno juu yenu,
Na kuwatikisia ninyi kichwa changu.
5Lakini ningewatia nguvu kwa kinywa changu,
Na maliwazo ya midomo yangu yangewatuliza.
6Nijapokuwa nanena, huzuni yangu haitulizwi;
Nijapokuwa najizuia, nimepunguziwa kitu gani?
7Lakini sasa amenichokesha;
Jamii yangu yote umeifanya ukiwa.
8Umenishika sana, na kuwa ushahidi juu yangu;
Na kukonda kwangu kwaniinukia, kwanishuhudia usoni pangu.
9Amenirarua katika ghadhabu zake, na kunionea;
Amesagasaga meno juu yangu;
Mtesi wangu hunikazia macho makali.
10Wamenifumbulia vinywa vyao;[#Zab 22:13; 1 Fal 22:24; Omb 3:30; Mik 5:1; Mt 26:67; Yn 18:22; Mdo 23:2; Zab 35:15]
Wamenipiga shavuni kwa kunitukana;
Hukutana pamoja juu yangu.
11Mungu amenitia kwa hao wapotovu,
Na kunitupa mikononi mwao waovu.
12Nilikuwa katika raha, naye akanivunjavunja;
Naam, amenishika shingo, na kuniponda;
Tena amenisimamisha niwe shabaha yake.
13Wapigaji wake wa mishale hunizingira kotekote,
Hunipasua figo zangu, asinihurumie;
Nyonga zangu amezimwaga juu ya nchi.
14Hunivunja kwa uvunjifu juu ya uvunjifu;
Hunishambulia mfano wa jitu shujaa.
15Nimeshona nguo ya magunia juu ya mwili wangu,[#Zab 7:5]
Na nguvu zangu nimezibwaga mavumbini.
16Uso wangu umeharibika kwa kutoa machozi,
Na giza tupu liko katika kope zangu;
17Ijapokuwa hakuna udhalimu mikononi mwangu,
Na kuomba kwangu ni safi.
18Ee nchi, usiifunike damu yangu,[#Ayu 27:9]
Na kilio changu kisipate mahali pa kupumzika.
19Hata sasa, tazama, shahidi wangu yuko mbinguni.[#Ayu 19:25; Rum 1:9]
Na huyo atakayenidhamini yuko juu.
20Rafiki zangu hunidharau;
Lakini jicho langu humwagia Mungu machozi;
21Laiti angemtolea mtu hoja mbele ya Mungu,[#Ayu 31:35]
Amtetee na mwanadamu mbele ya jirani yake.
22Kwani ikiisha pita miaka michache,[#Mhu 12:5]
Nitakwenda njia hiyo ambayo sitarudi tena.