The chat will start when you send the first message.
1Lakini sasa hao walio wadogo wangu hunifanyia mzaha,
Ambao baba zao ningewadharau hata kuwasimamia mbwa wa kundi langu.
2Naam, uwezo wa mikono yao utanifaa nini?
Watu ambao nguvu zao zimekoma.
3Wamekonda kwa uhitaji na njaa;
Huguguna nchi kavu, penye giza la ukiwa na uharibifu.
4Hung'oa mboga ya chumvi kwenye kichaka;
Na mizizi ya mretemu ni chakula chao.
5Hufukuzwa watoke kati ya watu;
Huwapigia kelele kama kumpigia mwizi.
6Lazima hukaa katika mianya ya mabonde,
Katika mashimo ya nchi na ya majabali.
7Hulia kama punda vichakani;
Hukusanyika chini ya upupu.
8Wao ni wana wa wapumbavu, naam, watoto wa wahuni;
Walifukuzwa kwa mijeledi watoke katika nchi.
9Na sasa mimi nimekuwa wimbo wao,[#Ayu 17:6; Zab 35:15; 69:11]
Naam, nimekuwa simo kwao.
10Wao hunichukia, na kujitenga nami,
Hawaachi kunitemea mate usoni.
11Kwani ameilegeza kamba yake, na kunitesa,[#Ayu 12:18]
Wala hawajizuii tena mbele yangu.
12Kwa mkono wangu wa kulia huinuka kundi;[#Ayu 19:12]
Huisukuma miguu yangu kando,
Na kunipandishia njia zao za uharibifu.
13Waiharibu njia yangu,[#Zab 69:26]
Wauzidisha msiba wangu,
Watu wasio na msaidizi.
14Wanijia kama wapitao katika ufa mpana;[#Zab 18:4; 69:14,15; Isa 8:7,8]
Katikati ya magofu wanishambulia.
15Vitisho vimenigeukia;
Huifukuza heshima yangu kama upepo;
Na kufanikiwa kwangu kumepita kama wingu.
16Sasa nafsi yangu inamwagika ndani yangu;[#1 Sam 1:15; Isa 53:12; Zab 22:14; 42:4]
Siku za mateso zimenishika.
17Wakati wa usiku mifupa yangu huchomeka ndani yangu,[#Ayu 33:19-21; Zab 6:2]
Na maumivu yanayonitafuna hayapumziki.
18Kwa ugonjwa wangu kuwa na nguvu nyingi[#Ayu 2:7]
Mavazi yangu yameharibika;
Hunikaza kama shingo ya kanzu yangu.
19Yeye amenibwaga topeni,
Nami nimekuwa kama mavumbi na majivu.
20Nakulilia wewe, wala huniitikii;[#Zab 22:2; Mt 15:23]
Nasimama, nawe wanitazama tu.
21Wewe umegeuka kuwa mkali kwangu;
Nawe waniudhi kwa uweza wa mkono wako.
22Waniinua juu hata upeponi, na kunipandisha juu yake;
Nawe waniyeyusha katika dhoruba.
23Kwani najua kuwa utanileta hata kifoni,
Niifikie nyumba waliyoaandaliwa wenye uhai wote.
24Je! Mtu katika kuanguka kwake hanyoshi mkono?
Na kulilia msaada katika msiba wake?
25Je! Mimi sikulia kwa ajili ya huyo aliyekuwa katika taabu?[#Lk 19:41; Yn 11:35; Rum 12:15]
Nafsi yangu, je! Haikusononeka kwa ajili ya wahitaji?
26Hapo nilipotazamia mema, ndipo yakaja mabaya;[#Yer 8:15]
Nami nilipongojea mwanga, likaja giza.
27Matumbo yangu yatokota, wala hayaachi;
Siku za taabu zimenijia.
28Naenda nikiomboleza pasipo jua;[#Omb 3:1,2]
Nasimama katika mkutano, na kuulilia msaada.
29Mimi ni ndugu yao mbwamwitu,[#Zab 102:6]
Ni mwenzao mbuni.
30Ngozi yangu ni nyeusi, nayo yanitoka,
Na mifupa yangu imeteketea kwa joto.
31Kwa hiyo kinanda changu kimegeuzwa kuwa maombolezo,
Na filimbi yangu kuwa sauti yao waliao.