Ayubu 35

Ayubu 35

Elihu alaani haki ya ubinafsi

1Tena Elihu akajibu na kusema,

2Je! Wewe wadhani kwamba haya ni haki yako,

Au je! Wasema, Ni haki yangu mbele za Mungu,

3Maana wasema, Kutakuwa na faida gani kwako wewe?

Tena, Nitapata faida gani, kuliko nikifanya dhambi?

4Mimi nitakujibu,

Na hawa wenzio pamoja nawe.

5Ziangalie mbingu ukaone;

Na mawingu yaangalie, yaliyo juu kuliko wewe.

6Ikiwa umefanya dhambi, umefanya nini juu yake?[#Ayu 22:2-3]

Ikiwa makosa yako yameongezeka, wamfanyia nini yeye?

7Ikiwa u mwenye haki, wampa kitu gani?[#Mit 9:12; Rum 11:35]

Au yeye hupokea nini mkononi mwako?

8Uovu wako waweza kumwumiza mtu kama wewe;

Na haki yako yaweza kumfaa mwanadamu.

9Kwa sababu ya wingi wa dhuluma wao hulia;[#Kut 2:23; Neh 5:5; Ayu 24:12; Zab 12:5; Lk 18:3-7]

Walilia msaada kwa sababu ya mkono wa wakuu.

10Wala hapana asemaye, Yuko wapi Mungu Muumba wangu,[#Mhu 12:1; Isa 51:13; 1 Pet 4:19; Zab 42:8; Mdo 16:25]

Awapaye nyimbo wakati wa usiku;

11Atufundishaye zaidi ya wanyama wa nchi,[#Ayu 32:8; Zab 8:6; 1 Yoh 5:20]

Na kutufanya wenye hekima kuliko ndege wa angani?

12Hulia huko, lakini hapana ajibuye,[#Mit 1:28]

Kwa sababu ya kiburi cha watu waovu.

13Hakika Mungu hatasikia ubatili,

Wala Mwenyezi hatauangalia.

14Sembuse usemapo wewe ya kuwa humwangalii,

Hiyo kesi i mbele yake, nawe wamngojea!

15Lakini sasa, kwa sababu yeye hakukujia katika hasira zake,

Wala hauzingatii sana makosa;

16Ndiposa Ayubu hufunua kinywa chake kwa ubatili;[#Ayu 34:35,37]

Huongeza maneno pasipo maarifa.

Swahili Revised Union Version Bible © Bible Society of Kenya, and Bible Society of Tanzania, 2005.
Published by: Bible Society of Kenya