The chat will start when you send the first message.
1Kisha BWANA akanena na Musa, na kumwambia,
2Tena uwaambie wana wa Israeli, Mtu yeyote miongoni mwa wana wa Israeli, au miongoni mwa wageni waishio katika Israeli, atakayetoa katika kizazi chake na kumpa Moleki, sharti atauawa; wenyeji wa nchi watampiga kwa mawe.[#2 Fal 17:17; 23:10; 2 Nya 33:6]
3Mimi nami nitamkazia uso wangu mtu huyo, na nitamtenga na watu wake; kwa kuwa ametoa katika kizazi chake na kumpa Moleki, ili kupatia unajisi patakatifu pangu, na kulinajisi jina langu takatifu.[#Eze 5:11; 23:38,39; Hes 19:20]
4Tena kama wenyeji wa nchi wakimfumbia macho mtu huyo kwa njia yoyote, hapo atoapo katika kizazi chake na kumpa Moleki, wasimwue;
5ndipo mimi nitamkazia uso wangu mtu huyo, na jamaa zake, nami nitamtenga na hao wote wamwandamao katika uzinifu, ili kufanya uzinifu pamoja na Moleki, watengwe mbali na watu wao.[#Kut 20:5; Law 17:7]
6Na mtu yule atakayewaendea wenye pepo, na wachawi, ili kuzini pamoja nao, nitakaza uso wangu juu ya mtu yule, nitamtenga na watu wake.[#Law 19:31; 2 Fal 23:24]
7Jitakaseni basi, kuweni watakatifu, kwa kuwa mimi ndimi BWANA, Mungu wenu.[#Kut 22:31; Mt 5:48; Efe 1:4; Kol 3:12; 1 The 5:23; 1 Pet 1:16]
8Nanyi zishikeni sheria zangu, na kuzitenda; Mimi ndimi BWANA niwatakasaye.[#Kut 31:13; Eze 37:28]
9Kwa maana kila mtu amlaaniye baba yake au mama yake hakika atauawa, amemlaani baba yake na mama yake; damu yake itakuwa juu yake.[#Kut 21:17; Mt 15:4; Mk 7:10; Kum 27:16; Mit 20:20; 2 Sam 1:16; 1 Fal 2:32]
10Na mtu aziniye na mke wa mtu mwingine, yeye aziniye na mke wa jirani yake, mwanamume aziniye, na mwanamke aziniye, hakika watauawa.[#Kut 20:14; Law 18:20; Kum 5:18; 22:22; Yer 29:23; Yn 8:4,5; 1 Kor 6:9; Ebr 13:4]
11Na mwanamume atakayelala pamoja na mke wa baba yake amefunua utupu wa baba yake; wote wawili hakika watauawa; damu yao itakuwa juu yao.[#Law 18:8; Kum 22:30; 27:20,23]
12Na mwanamume akilala na mkwewe mwanamke, wote wawili hakika watauawa; wamefanya yaliyo upotovu; damu yao itakuwa juu yao.[#Law 18:15]
13Tena mwanamume akilala pamoja na mwanamume, kama alalavyo na mwanamke, wote wawili wamefanya machukizo; hakika watauawa; damu yao itakuwa juu yao.[#Law 18:22; Mwa 19:5; Rum 1:25,32]
14Tena mwanamume akimwoa mke pamoja na mama yake, ni uovu mkuu; watachomwa moto, yeye mume na hao wanawake pia; ili kwamba usiwe uovu kati yenu.[#Law 18:17; Kum 27:23]
15Tena mwanamume akilala na mnyama, hakika atauawa; nanyi mtamwua huyo mnyama.[#Kut 22:19; Law 18:23; Kum 27:21]
16Tena mwanamke akimmwendea mnyama yeyote, na kulala pamoja naye, mtamwua huyo mwanamke, na mnyama pia; hakika watauawa; damu yao itakuwa ni juu yao.
17Tena mwanamume akimwoa dada yake, binti ya baba yake, au binti ya mama yake, na kuuona utupu wake, na huyo mwanamke kauona utupu wake huyo mwanamume; ni jambo la aibu; watengwa mbele ya macho ya wana wa watu wao; amefunua utupu wa dada yake; naye atauchukua uovu wake.[#Law 18:9; Kum 27:22; Mwa 20:12]
18Tena mwanamume akilala na mwanamke aliye na ugonjwa wake, na kufunua utupu wake; amefunua jito la damu yake, naye mwanamke amefunua jito la damu yake; wote wawili watatengwa mbali na watu wao.[#Law 18:19; 15:24; #20:18 Au hedhi.]
19Usifunue utupu wa dada ya mama yako, wala dada ya baba yako; kwa kuwa huyo amefunua utupu wa jamaa yake ya karibu; watalipizwa kwa uovu wao.[#Law 18:12-14]
20Tena mwanamume akilala na mke wa mjomba wake, ameufunua utupu wa mjomba wake; watauchukua uovu wao; watakufa bila kuzaa mwana.
21Tena mwanamume akimtwaa mke wa nduguye, ni upotovu; ameufunua utupu wa nduguye; hao watakuwa hawana wana.[#Law 18:16]
22Basi zishikeni amri zangu zote, na maagizo yangu yote, na kuzifanya; ili kwamba hiyo nchi, ambayo nawapeleka ninyi kukaa, isiwatapike.[#Law 18:26; 19:37]
23Nanyi msiende kwa kuzifuata desturi za taifa, niitoayo mbele yenu; kwa kuwa wao waliyafanya mambo hayo yote, na kwa ajili ya hayo niliwachukia.[#Kum 9:5]
24Lakini mimi nimewaambia ninyi, Mtairithi nchi yao, nami nitawapa ninyi kuimiliki; nchi iliyojaa maziwa na asali; mimi ni BWANA, Mungu wenu, niliyewatenga ninyi na mataifa.[#Kut 3:17; 6:8; 19:5; 33:16; Kum 7:6; 14:2; 1 Fal 8:53; Zab 135:4; 1 Pet 2:9]
25Kwa ajili ya hayo mtapambanua kati ya mnyama aliye safi na mnyama aliye najisi, na kati ya ndege aliye safi na ndege aliye najisi; nanyi msizifanye nafsi zenu kuwa machukizo kwa njia ya mnyama, au kwa njia ya ndege, au kwa njia ya kitu chochote ambacho nchi imejaa nacho, nilichokitenga nanyi kuwa ni najisi.[#Law 11:47; Kum 14:4; #20:25 Au tohara.]
26Nanyi mtakuwa watakatifu kwangu; kwa kuwa mimi BWANA ni mtakatifu nami nimewatenga ninyi na mataifa, ili kwamba muwe wangu.[#Law 19:2; Zab 99:5; Isa 6:3; 30:11; 1 Pet 1:16; Ufu 3:7; 4:8; Tit 2:14]
27Tena mwanamume au mwanamke aliye na pepo, au aliye mchawi, hakika atauawa; watawapiga kwa mawe; damu yao itakuwa juu yao.[#Kut 22:18; Kum 18:10; 1 Sam 28:7]