The chat will start when you send the first message.
1Kwa maana, angalieni, siku ile inakuja, inawaka kama tanuri; na watu wote wenye kiburi, nao wote watendao uovu, watakuwa makapi; na siku ile inayokuja itawateketeza, asema BWANA wa majeshi; hata haitawaachia shina wala tawi.[#4:1 Kwa maana, Sura ya 4:1-6 ni Sura 3:19-24 katika Kiebrania.]
2Lakini kwenu ninyi mnaolicha jina langu, jua la haki litawachomozea, likiwa na uwezo wa kuponya katika miale yake; nanyi mtatoka nje, na kuchezacheza kama ndama watokapo mazizini.[#Lk 1:78; Efe 5:14; 2 Pet 1:19]
3Nanyi mtawakanyaga waovu; maana watakuwa majivu chini ya nyayo za miguu yenu; katika siku ile niifanyayo, asema BWANA wa majeshi.[#Mik 7:10]
4Ikumbukeni Torati ya Musa, mtumishi wangu, niliyomwamuru huko Horebu kwa ajili ya Israeli wote, naam, amri na hukumu.[#Kum 4:10]
5Angalieni, nitawatumia Eliya nabii, kabla siku ile ya BWANA, iliyo kuu na ya kuogofya haijafika.[#Yoe 2:31; Mt 11:14; 17:10-13; Mk 9:11-13; Lk 1:17; Yn 1:21]
6Naye ataigeuza mioyo ya baba iwaelekee watoto wao, na mioyo ya watoto iwaelekee baba zao, ili nisije nikaipiga dunia kwa laana.[#Lk 1:17; Dan 9:26; Lk 19:27,43; 21:20; Mk 13:14]