Nehemia 10

Nehemia 10

1Basi hawa ndio waliotia mhuri; Nehemia, ndiye Tirshatha, mwana wa Hakalia, na Sedekia;[#Neh 8:9; 1:1]

2Seraya, Azaria, Yeremia;

3Pashuri, Amaria, Malkiya;

4Hamshi, Shekania, Maluki;

5Harimu, Meremothi, Obadia;

6Danieli, Ginethoni, Baruku;

7Meshulamu, Abiya, Miyamini;

8Maazia, Bilgai, Shemaya; hao ndio waliokuwa makuhani.

9Na Walawi; ndio, Yeshua, mwana wa Azania, Binui wa wana wa Henadadi, Kadmieli;[#Neh 12:8]

10na ndugu zao, Shebania, Hodia, Kelita, Pelaya, Hanani;

11Mika, Rehobu, Hashabia;

12Zakuri, Sherebia, Shebania;

13Hodia, Bani, Beninu;

14Na viongozi wa watu; Paroshi, Pahath-Moabu, Elamu, Zatu, Bani;

15Buni, Azgadi, Bebai;

16Adonikamu, Bigwai, Adini;

17Ateri, Hezekia, Azuri;

18Hodia, Hashumu, Besai;

19Harifu, Anathothi, Nobai;

20Magpiashi, Meshulamu, Heziri;

21Meshezabeli, Sadoki, Yadua;

22Pelatia, Hanani, Anaya;

23Hoshea, Hanania, Hashubu;

24Haloheshi, Pilha, Shobeki;

25Rehumu, Hashabna, Maaseya;

26Ahia, Hanani, Anani;

27Maluki, Harimu, na Baana.

Muhtasari wa Agano

28Na watu waliosalia, makuhani, Walawi, mabawabu, waimbaji, Wanethini, na hao wote waliojitenga katika watu wa nchi kwa Torati ya Mungu; wake zao, na wana wao, na binti zao, kila mwenye maarifa na akili;[#Ezr 2:36; 9:1; Neh 13:3]

29wakaambatana na ndugu zao, wakuu wao, nao wakaingia katika laana na kiapo, ya kuwa wataiendea Torati ya Mungu, iliyotolewa kwa mkono wa Musa, mtumishi wa Mungu, na kuziangalia, na kuzitenda, amri zote za BWANA, Bwana wetu, na maagizo yake na sheria zake;[#Kum 29:12; Neh 5:12; Isa 14:1; Rum 12:9; 2 Fal 23:3]

30wala tusiwaoze watu wa nchi binti zetu, wala kuwatwalia wana wetu binti zao;[#Mwa 6:2; Kut 34:16; Kum 7:3]

31tena watu wa nchi wakitembeza biashara, au chakula chochote, siku ya sabato, tusinunue kwao siku ya sabato, au siku takatifu; tena mwaka wa saba tusiliwe na madeni yote tuyafute.[#Kut 20:10; Law 23:3; Neh 13:15; Yer 17:21; Kut 23:10; Law 25:4; Kum 15:1; Neh 5:12]

32Tena tukajifanyia maagizo, kujitoza mwaka kwa mwaka theluthi ya shekeli kwa huduma ya nyumba ya Mungu wetu;[#Mwa 28:22]

33kwa mikate mitakatifu, na kwa sadaka ya unga ya daima, na kwa sadaka ya kuteketezwa ya daima, ya sabato, na ya siku za mwezi mpya, na ya sikukuu, tena kwa vitu vile vitakatifu, na kwa sadaka za dhambi, za kuwafanyia Israeli upatanisho, na kwa ajili ya kazi yote ya nyumba ya Mungu wetu.[#Law 24:5; 2 Nya 2:4]

34Kisha tukapiga kura, makuhani, na Walawi, na watu, juu ya matoleo ya kuni, ili kuzileta nyumbani kwa Mungu wetu, kwa kadiri ya mbari za baba zetu, kwa nyakati zilizoamriwa, mwaka kwa mwaka, kukoka moto madhabahuni mwa BWANA, Mungu wetu, kama ilivyoandikwa katika torati;[#Neh 13:31; Law 6:12]

35tena kuleta malimbuko ya ardhi yetu, na malimbuko ya matunda yote ya miti ya namna zote, mwaka kwa mwaka, nyumbani kwa BWANA;[#Kut 23:19; Law 19:23; Hes 18:12; Kum 26:2]

36tena wazaliwa wa kwanza wa wana wetu, na wa wanyama wetu, kama ilivyoandikwa katika torati, na wazaliwa wa kwanza wa ng'ombe wetu na kondoo wetu, ili kuwaleta nyumbani mwa Mungu wetu, kwa makuhani watumikao nyumbani mwa Mungu wetu;[#Kut 13:2,12,13; Law 27:26,27]

37tena tuyalete malimbuko ya unga wetu, na matoleo yetu, na matunda ya miti ya namna zote, mvinyo, na mafuta, kwa makuhani, hapo vyumbani kwa nyumba ya Mungu wetu; na zaka za ardhi yetu kwa Walawi; kwa kuwa hao Walawi ndio wanaozitwaa zaka vijijini kwetu kote.[#Law 23:17; Hes 15:19; Kum 18:4; Law 27:30; 2 Nya 31:6]

38Naye kuhani, mwana wa Haruni, atakuwako pamoja na Walawi, watwaapo zaka Walawi; nao Walawi wataipandisha zaka ya hizo zaka nyumbani kwa Mungu wetu, vyumbani, katika nyumba ya hazina.[#Hes 18:26; 1 Nya 9:26; 2 Nya 31:11]

39Kwa kuwa wana wa Israeli na wana wa Lawi wataleta sadaka ya kuinuliwa ya nafaka, na mvinyo, na mafuta, vyumbani, kwa kuwa ndimo vilimo vyombo vya patakatifu, na makuhani watumikao, na mabawabu, na waimbaji; wala sisi hatutaiacha nyumba ya Mungu wetu.[#Hes 18:30; Kum 12:6; Neh 13:10-12; Zab 122:9; Mt 18:20]

Swahili Revised Union Version Bible © Bible Society of Kenya, and Bible Society of Tanzania, 2005.
Published by: Bible Society of Kenya