The chat will start when you send the first message.
1Ikawa, baada ya ukuta kujengwa, na milango kuisimamishwa na kuweka mabawabu, waimbaji na Walawi,[#Neh 3:1-32; 6:1]
2ndipo nilimteua ndugu yangu Hanani, kuwa mwangalizi wa Yerusalemu akisaidiana na Hanania, jemadari wa ngome, kwa maana alikuwa mtu mwaminifu na mwenye kumcha Mungu kuliko wengi.[#Hes 12:7; Zab 101:6; Mt 24:45; 1 Kor 4:2; Mwa 42:18; Kut 18:21; Ayu 31:23; Mit 16:6]
3Nikawaambia, Yasifunguliwe malango ya Yerusalemu kabla jua halijachomoza; na kabla walinzi hawajaondoka waifunge milango, mkaikaze; kisha wekeni walinzi wa zamu wa hao wakaao Yerusalemu, kila mtu na zamu yake, na kila mtu kuielekea nyumba yake.
4Basi mji ulikuwa wa nafasi nyingi, tena mkubwa; lakini watu waliomo walikuwa wachache, na nyumba zilikuwa hazijajengwa.
5Mungu wangu akanitia moyoni mwangu, kwamba niwakusanye wakuu na maofisa, na watu, ili wahesabiwe kwa nasaba.[#Mit 2:6; Rum 11:36; 1 Kor 4:7; 2 Kor 8:16; Yak 1:17]
Nikakiona kitabu cha vizazi vya hao waliokwea hapo kwanza, nikaona ya kwamba imeandikwa humo;
6Hawa ndio wana wa wilaya, waliokwea kutoka katika ule uhamisho wa hao waliokuwa wamechukuliwa, ambao Nebukadneza, mfalme wa Babeli, aliwachukua mateka, nao wakarudi Yerusalemu na Yuda, kila mtu mjini kwake;[#Ezr 2:1-70; #7:6 Makala nyingine ni ‘Nebukadneza’.]
7ndio hawa waliokuja pamoja na Zerubabeli, Yoshua, Nehemia, Seraya, Reelaya, Nahamani, Mordekai, Bilshani, Mispari, Bigwai, Rehumu, na Baana. Hii ndiyo idadi ya watu wa watu wa Israeli;[#Ezr 2:2]
8Wana wa Paroshi, elfu mbili mia moja sabini na wawili.
9Wana wa Shefatia, mia tatu sabini na wawili.
10Wana wa Ara mia sita hamsini na wawili.
11Wana wa Pahath-Moabu, wa wana wa Yeshua na Yoabu, elfu mbili mia nane na kumi na wanane.
12Wana wa Elamu, elfu moja mia mbili hamsini na wanne.
13Wana wa Zatu, mia nane arubaini na watano.
14Wana wa Zakai, mia saba na sitini.
15Wana wa Binui, mia sita arubaini na wanane.
16Wana wa Bebai, mia sita ishirini na wanane.
17Wana wa Azgadi, elfu mbili mia tatu ishirini na wawili.
18Wana wa Adonikamu, mia sita sitini na saba.
19Wana wa Bigwai, elfu mbili sitini na saba.
20Wana wa Adini, mia sita hamsini na watano.
21Wana wa Ateri, wa Hezekia, tisini na wanane.
22Wana wa Hashumu, mia tatu ishirini na wanane.
23Wana wa Besai, mia tatu ishirini na wanne.
24Wana wa Harifu, mia moja na kumi na wawili.
25Wana wa Gibeoni, tisini na watano.
26Watu wa Bethlehemu na Netofa, mia moja na themanini na wanane.[#Mwa 35:6; Rut 2:4; 1 Sam 17:12; 2 Nya 11:6; Mik 5:2; Mt 2:1]
27Watu wa Anathothi, mia moja ishirini na wanane.[#Yos 21:18; 1 Nya 6:54,60; Ezr 2:23; Yer 1:1]
28Watu wa Beth-Azmawethi, arubaini na wawili.
29Watu wa Kiriath-Yearimu, na Kefira, na Beerothi, mia saba arubaini na watatu.
30Watu wa Rama na Geba, mia sita na ishirini na mmoja.
31Watu wa Mikmashi, mia moja na ishirini na wawili.[#1 Sam 13:2; Isa 10:28]
32Watu wa Betheli na Ai, mia moja ishirini na watatu.
33Watu wa Nebo, hamsini na wawili.
34Wana wa Elamu wa pili, elfu moja mia mbili hamsini na wanne.
35Wana wa Harimu, mia tatu na ishirini.
36Wana wa Yeriko, mia tatu arubaini na watano.
37Wana wa Lodi, na Hadidi, na Ono, mia saba ishirini na mmoja.
38Watu wa Senaa, elfu tatu mia tisa na thelathini.
39Makuhani; Wana wa Yedaya, wa mbari ya Yeshua, mia tisa sabini na watatu.[#1 Nya 24:7]
40Wana wa Imeri, elfu moja hamsini na wawili.[#1 Nya 24:14]
41Wana wa Pashuri, elfu moja mia mbili arubaini na saba.[#1 Nya 9:12; 24:9]
42Wana wa Harimu, elfu moja na kumi na saba.[#1 Nya 24:8; Ezr 10:31]
43Walawi; Wana wa Yeshua, wa Kadmieli wa wana wa Hodavia, sabini na wanne.
44Waimbaji; Wana wa Asafu, mia moja arubaini na wanane.
45Mabawabu; Wana wa Shalumu, wana wa Ateri, wana wa Talmoni, wana wa Akubu, wana wa Hatita, wana wa Shobai, mia moja thelathini na wanane.
46Wanethini; wana wa Siha, wana wa Hasufa, wana wa Tabaothi;
47wana wa Kerosi, wana wa Siaha, wana wa Padoni;
48wana wa Lebana, wana wa Hagaba, wana wa Salmai;
49wana wa Hanani, wana wa Gideli, wana wa Gahari;
50wana wa Reaya, wana wa Resini, wana wa Nekoda;
51wana wa Gazamu, wana wa Uza, wana wa Pasea;
52wana wa Besai wana wa Meunimu, wana wa Nefusimu;
53wana wa Bakbuki, wana wa Hakufa, wana wa Harhuri;
54wana wa Basluthi, wana wa Mehida, wana wa Harsha;
55wana wa Barkosi, wana wa Sisera, wana wa Tema;
56wana wa Nesia, wana wa Hatifa.
57Wazawa wa watumishi wa Sulemani; Wana wa Sotai, wana wa Soferethi, wana wa Peruda;[#Mwa 9:25,26; 1 Fal 5:13,14; 2 Nya 2:17,18]
58wana wa Yaala, wana wa Darkoni, wana wa Gideli;
59wana wa Shefatia, wana wa Hatili, wana wa Pokereth-Sebaimu, wana wa Amoni.
60Wanethini wote, pamoja na wazawa wa watumishi wa Sulemani, walikuwa mia tatu tisini na wawili.
61Na hawa ndio watu waliokwea kutoka Tel-mela, na Tel-harsha, na Kerubu, na Adani, na Imeri; lakini hawakuweza kuonesha mbari za baba zao, wala kizazi chao, kwamba walikuwa wa Israeli;[#Ezr 2:59]
62Wana wa Delaya, wana wa Tobia, wana wa Nekoda, mia sita na arubaini na wawili.
63Tena katika makuhani; Wana wa Habaya, wana wa Hakosi, wana wa Barzilai, yule aliyeoa mmojawapo wa binti za Barzilai, Mgileadi, akaitwa kwa jina lao.[#2 Sam 17:27; 19:31-34; 1 Fal 2:7; Ezr 2:61]
64Hao waliitafuta orodha yao miongoni mwa wale waliohesabiwa kwa nasaba, wasionekane; kwa hiyo walihesabiwa kuwa na unajisi.
65Na huyo Tirshatha akawaambia kwamba wasile katika vile vitu vitakatifu sana, hata atakaposimama kuhani mwenye Urimu na Thumimu.[#Kut 28:30; Law 8:8; Hes 7:89; 27:18-21; Kum 33:8; Amu 1:1; #7:65 Tazama Ezr 2:63.]
66Basi hilo kusanyiko lote zima, jumla yake ilikuwa watu elfu arubaini na mbili, mia tatu na sitini,
67tena zaidi ya hao, kulikuwa na watumishi wao wanaume kwa wanawake, ambao walikuwa elfu saba na mia tatu na thelathini na saba; kisha walikuwa na waimbaji wanaume kwa wanawake mia mbili arubaini na watano.
68Farasi wao walikuwa mia saba thelathini na sita; nyumbu zao, mia mbili arubaini na watano;
69ngamia wao, mia nne thelathini na watano; punda zao, elfu sita na mia saba na ishirini.
70Na baadhi ya wakuu wa mbari za mababa walitoa mali kwa ajili ya kazi hii. Yule Tirshatha akatoa kwa ajili ya hazina darkoni, za dhahabu elfu moja, na mabeseni hamsini, na mavazi ya makuhani mia tano na thelathini.[#Neh 8:9; 10:1; #7:70 Tazama Neh 7:65.; #7:70 ni sarafu, ambayo thamani yake ni kama dola 5 za Kimarekani.]
71Na baadhi ya wakuu wa mbari za mababa wakatoa, na kutia katika hazina ya kazi hiyo, darkoni za dhahabu elfu ishirini, na mane za fedha elfu mbili na mia mbili.[#Ezr 2:69; #7:71 Ni kipimo cha uzito. Mane moja ni kama wakia 20 Ibs 1 na Oz. 4 = ratili moja na robo.]
72Na mabaki ya watu wakatoa darkoni za dhahabu elfu ishirini, na mane za fedha elfu mbili, na mavazi ya makuhani sitini na saba.[#Ayu 34:10; Rum 2:11; Gal 3:28]
73Hivyo makuhani, na Walawi, na mabawabu, na waimbaji, na baadhi ya watu, na Wanethini, na Israeli wote, wakakaa mijini mwao.[#Neh 11:20; Kut 23:14-17; Law 23:24-44; Ezr 3:1]
Hata ulipowadia mwezi wa saba, wana wa Israeli walikuwa wakikaa katika miji yao.