The chat will start when you send the first message.
1Ikawa baada ya hilo pigo, BWANA akanena na Musa na Eleazari, mwana wa Haruni kuhani, na kuwaambia,[#Hes 1:1-46]
2Fanya hesabu ya jumuiya yote ya wana wa Israeli, tangu umri wa miaka ishirini, na zaidi, kwa nyumba za baba zao, hao wote katika Israeli wawezao kutoka kuenenda vitani.[#Kut 30:12; 38:25; Hes 1:2]
3Kisha Musa na Eleazari kuhani wakanena nao katika nchi tambarare za Moabu karibu na mto wa Yordani, huko Yeriko, wakawaambia,[#Kum 4:46-49; 34:1]
4Fanyeni hesabu ya watu, kuanzia umri wa miaka ishirini, na zaidi; kama BWANA alivyomwagiza Musa na wana wa Israeli, hao waliotoka nchi ya Misri.
5Reubeni mzaliwa wa kwanza wa Israeli, wana wa Reubeni; wa Hanoki, jamaa ya Wahanoki; na wa Palu, jamaa ya Wapalu;[#Mwa 29:32; 46:8; 1 Nya 5:1; Ufu 7:5]
6na wa Hesroni, jamaa ya Wahesroni; na wa Karmi, jamaa ya Wakarmi.
7Hizi ndizo jamaa za Wareubeni; na hao waliohesabiwa kwao walikuwa elfu arubaini na tatu, mia saba na thelathini.
8Na wana wa Palu; Eliabu.
9Na wana wa Eliabu; Nemueli, na Dathani, na Abiramu. Hawa ndio Dathani na Abiramu waliochaguliwa na mkutano, ambao walishindana na Musa na Haruni katika mkutano wa Kora, hapo waliposhindana na BWANA;[#Hes 16:1,2; 27:3; Kum 11:6; Isa 65:16; Zab 106:17; Yud 1:11]
10nchi ikafunua kinywa chake, na kuwameza pamoja na Kora, mkutano huo ulipokufa; wakati moto ulipowateketeza watu mia mbili na hamsini, nao wakawa ishara.[#Hes 16:38; 1 Sam 2:34; Ayu 31:3; Zab 145:20; Yer 29:22; 1 Kor 10:6; 2 Pet 2:6; Yud 1:7]
11Hata hivyo, hao wana wa Kora hawakufa.[#Kut 6:24; 1 Nya 6:22; Eze 18:20]
12Na wana wa Simeoni kwa jamaa zao; wa Yemueli, jamaa ya Wayemueli; wa Yamini, jamaa ya Wayamini; na Yakini, jamaa ya Wayakini;[#Mwa 46:10; Kut 6:15; 1 Nya 4:24]
13wa Sohari, jamaa ya Wasohari; wa Shauli, jamaa ya Washauli.[#Mwa 46:10]
14Hawa ndizo jamaa wa Wasimeoni, watu elfu ishirini na mbili na mia mbili.
15Na wana wa Gadi kwa jamaa zao; wa Sifoni, jamaa ya Wasifoni; wa Hagi, jamaa ya Wahagi; wa Shuni, jamaa ya Washuni;
16wa Ezboni, jamaa ya Waezboni; wa Eri, jamaa ya Waeri;
17wa Arodi, jamaa ya Waarodi; wa Areli, jamaa ya Waareli.[#Mwa 46:16]
18Hawa ndio jamaa wa wana wa Gadi kama waliohesabiwa kwao, elfu arubaini na mia tano.
19Na wana wa Yuda, Eri na Onani; na hao Eri na Onani wakafa katika nchi ya Kanaani.[#Mwa 38:2; 46:12; 1 Nya 2:3]
20Na wana wa Yuda kwa jamaa zao; wa Shela, jamaa ya Washela; wa Peresi, jamaa ya Waperesi; wa Zera, jamaa ya Wazera.[#Mwa 49:8; Ufu 7:5]
21Na wana wa Peresi walikuwa; wa Hesroni, jamaa ya Wahesroni; wa Hamuli, jamaa ya Wahamuli.
22Hawa ndio jamaa wa Yuda kama waliohesabiwa kwao, elfu sabini na sita na mia tano.
23Na wana wa Isakari kwa jamaa zao; wa Tola, jamaa ya Watola; wa Puva, jamaa ya Wapuva;[#Mwa 46:13; 49:14]
24wa Yashubu, jamaa ya Wayashubu; wa Shimroni, jamaa ya Washimroni.
25Hawa ndio jamaa wa Isakari kama waliohesabiwa kwao, elfu sitini na nne na mia tatu.
26Na wana wa Zabuloni kwa jamaa zao; wa Seredi, jamaa ya Waseredi; wa Eloni, jamaa ya Waeloni; wa Yaleeli, jamaa ya Wayaleeli.[#Mwa 46:14; 49:13]
27Hawa ndio jamaa wa Wazabuloni kama waliohesabiwa kwao, elfu sitini na mia tano.
28Na wana wa Yusufu kwa jamaa zao; Manase na Efraimu.[#Mwa 41:51; 46:20; 48:3,13-20]
29Wana wa Manase; wa Makiri, jamaa ya Wamakiri; na Makiri akamzaa Gileadi; wa Gileadi, jamaa ya Wagileadi.[#Hes 32:39; 36:1]
30Hawa ndio wana wa Gileadi; wa Abiezeri, jamaa ya Waabiezeri; wa Heleki, jamaa ya Waheleki;[#Yos 17:2]
31na wa Asrieli, jamaa ya Waasrieli; na wa Shekemu, jamaa ya Washekemu;
32na wa Shemida, jamaa ya Washemida; na wa Heferi, jamaa ya Waheferi.
33Na Selofehadi mwana wa Heferi hakuwa na watoto wa kiume, isipokuwa wa kike; na majina ya hao binti za Selofehadi ni haya, Mala, na Nuhu, na Hogla, na Milka, na Tirza.[#Hes 27:1; 36:11; Yos 17:3]
34Hawa ndizo jamaa wa Manase; na waliohesabiwa kwao walikuwa ni elfu hamsini na mbili na mia saba.
35Na wana wa Efraimu kwa jamaa zao; wa Shuthela, jamaa ya Washuthela; wa Beredi, jamaa ya Waberedi; wa Tahathi, jamaa ya Watahathi.[#1 Nya 7:20]
36Na wana wa Shuthela ni hawa; wa Erani, jamaa ya Waerani.
37Hawa ndio jamaa wa wana wa Efraimu kama waliohesabiwa kwao, elfu thelathini na mbili na mia tano. Hao ndio wana wa Yusufu kwa jamaa zao.[#Kum 33:13-17]
38Na wana wa Benyamini kwa jamaa zao; wa Bela, jamaa ya Wabela; na wa Ashbeli, jamaa ya Waashbeli; wa Ahiramu, jamaa ya Waahiramu;[#Mwa 46:21; 1 Nya 7:6; 8:1]
39wa Shufamu, jamaa ya Washufamu; wa Hufamu, jamaa ya Wahufamu.[#Mwa 46:21; 1 Nya 7:12]
40Na wana wa Bela walikuwa Ardi na Naamani; wa Ardi, jamaa ya Waardi; wa Naamani, jamaa ya Wanaamani.[#1 Nya 8:3]
41Hao ndio wana wa Benyamini kwa jamaa zao; na waliohesabiwa kwao walikuwa elfu arubaini na tano na mia sita.
42Na wana wa Dani ni hawa kwa jamaa zao; wa Shuhamu, jamaa ya Washuhamu. Hizi ndizo jamaa za Dani kwa jamaa zao.[#Mwa 46:23; 49:16; Hes 1:38,39; Kum 33:22]
43Jamaa zote za Washuhamu, kama waliohesabiwa kwao, walikuwa elfu sitini na nne na mia nne.
44Na wana wa Asheri kwa jamaa zao; wa Imna, jamaa ya Waimna; wa Ishvi jamaa ya Waishvi; wa Beria, jamaa ya Waberia.[#Mwa 46:17; 1 Nya 7:30]
45Wa wana wa Beria; wa Heberi, jamaa ya Waheberi; wa Malkieli, jamaa ya Wamalkieli.
46Na jina la binti wa Asheri aliitwa Sera.
47Hawa ndio jamaa wa wana wa Asheri kama waliohesabiwa kwao, elfu hamsini na tatu na mia nne.
48Na wana wa Naftali kwa jamaa zake; wa Yaseeli, jamaa ya Wayaseeli; na wa Guni, jamaa ya Waguni;[#Mwa 46:24; 1 Nya 7:13]
49wa Yeseri, jamaa ya Wayeseri, wa Shilemu jamaa ya Washilemu.[#1 Nya 7:13]
50Hawa ndio jamaa wa Naftali kwa jamaa zao; na waliohesabiwa kwao walikuwa elfu arubaini na tano na mia nne.
51Hao ndio waliohesabiwa katika wana wa Israeli, elfu mia sita na moja, mia saba na thelathini (601,730).[#1:46; 2:32]
52Kisha BWANA akanena na Musa, na kumwambia,[#Hes 34:13; Yos 14:1-2]
53Watu hawa watagawiwa nchi hiyo iwe urithi wao, kulingana na idadi yao ilivyo.
54Hao waliozidi hesabu yao utawapa urithi zaidi, na hao waliopunguka hesabu yao, utawapa urithi kama upungufu wao; kila mtu kama watu wake walivyohesabiwa, ndivyo atakavyopewa urithi wake.[#Hes 33:54]
55Lakini nchi itagawanywa kwa kura; kwa majina ya makabila ya baba zao, ndivyo watakavyopata urithi.[#Hes 34:13; Yos 11:23; 14:2]
56Kama kura itakavyokuwa, ndivyo urithi wao utakavyogawanywa kati yao, hao wengi na hao wachache.
57Na hao waliohesabiwa katika Walawi kwa jamaa zao ni hawa; wa Gershoni, jamaa ya Wagershoni; na wa Kohathi, jamaa ya Wakohathi; na wa Merari, jamaa ya Wamerari.[#Mwa 46:11; Kut 6:16; 1 Nya 6:1,16]
58Hizi ndizo jamaa za Lawi; jamaa ya Walibni, na jamaa ya Wahebroni, na jamaa ya Wamala, na jamaa ya Wamushi jamaa ya Wakora. Na Kohathi alimzaa Amramu.
59Na jina la mke wa Amramu aliitwa Yokebedi, binti wa Lawi, ambaye alizaliwa kwake Lawi huko Misri; na huyo Yokebedi akamzalia Amramu Haruni, na Musa, na Miriamu dada yao.
60Tena kwake Haruni walizaliwa hawa, Nadabu, na Abihu, na Eleazari, na Ithamari.[#Hes 3:2]
61Tena Nadabu na Abihu wakafa, hapo waliposongeza moto wa kigeni mbele za BWANA.[#Law 10:1-2; Hes 3:4; 1 Nya 24:2]
62Na hao waliohesabiwa kwao walikuwa elfu ishirini na tatu, kila mwanamume tangu huyo aliyepata umri wa mwezi mmoja, na zaidi; kwa kuwa hawakuhesabiwa katika wana wa Israeli, kwa sababu hawakupewa urithi katika wana wa Israeli.[#Hes 3:39; 1:49; 18:20-24; 35:2-8; Kum 10:9; 14:27-29; Yos 13:14; 14:3]
63Hao ndio waliohesabiwa na Musa na Eleazari kuhani; ambao waliwahesabu wana wa Israeli katika nchi tambarare za Moabu, karibu na Yordani, hapo Yeriko.
64Lakini katika watu hao hapakuwa na mtu hata mmoja wa wale waliohesabiwa na Musa na Haruni kuhani; waliowahesabu wana wa Israeli katika bara ya Sinai.[#Hes 1:1; Kum 2:14,15]
65Kwa kuwa BWANA alisema juu yao, Hapana budi watakufa nyikani. Napo hapakusalia mtu mmoja miongoni mwao, isipokuwa Kalebu mwana wa Yefune, na Yoshua mwana wa Nuni.[#Hes 14:26-35; Kum 32:49,50; Zab 90:3-8; Rum 11:22; 1 Kor 10:5; Ebr 3:17,18; Yud 1:5; Hes 14:30; 32:12; Kum 1:36,38; Yos 14:10]