The chat will start when you send the first message.
1Ndipo Bildadi, Mshuhi, akajibu, na kusema,
2Enzi na hofu zi pamoja naye;
Hufanya amani katika mahali pake palipoinuka.
3Je! Majeshi yake yahesabika?[#Mwa 1:3-5,14-16; Zab 19:4-6; 139:8,11; Mt 5:45; Yak 1:17]
Ni nani asiyetokewa na mwanga wake?
4Basi mtu awezaje kuwa na haki mbele ya Mungu?[#Ayu 4:17; 9:2; Zab 130:3; 143:2; Rum 3:19,20]
Au awezaje kuwa safi aliyezaliwa na mwanamke?
5Tazama, hata mwezi hauangazi,
Wala nyota si safi machoni pake;
6Siuze mtu, aliye mdudu![#Zab 22:6]
Na mwanadamu, ambaye ni buu!