Yon 2

Yon 2

Wimbo wa Kushukuru

1Ndipo Yona akamwomba BWANA, Mungu wake, katika tumbo la yule samaki,

2Akasema,

Nalimlilia BWANA kwa sababu ya shida yangu,

Naye akaniitikia;

Katika tumbo la kuzimu naliomba,

Nawe ukasikia sauti yangu.

3Maana ulinitupa vilindini,[#Zab 88:6]

Ndani ya moyo wa bahari;

Gharika ya maji ikanizunguka pande zote;

Mawimbi yako yote na gharika zako zote zimepita juu yangu.

4Nami nikasema, Nimetupwa mbali na macho yako;[#Zab 31:22; Isa 49:14; 1 Fal 8:38]

Lakini nitatazama tena kukabili hekalu lako takatifu.

5Maji yalinizunguka, hata nafsini mwangu;

Vilindi vilinizunguka;

Mwani ulikizinga kichwa changu;

6Nalishuka hata pande za chini za milima;

Hiyo nchi na mapingo yake yalinifunga hata milele;

Lakini umeipandisha nafsi yangu kutoka shimoni,

Ee BWANA, Mungu wangu,

7Roho yangu ilipozimia ndani yangu,[#Zab 18:6; 34:6; 130:2; Yer 2:13]

Nalimkumbuka BWANA;

Maombi yangu yakakuwasilia,

Katika hekalu lako takatifu.

8Watu waangaliao mambo ya ubatili na uongo[#2 Fal 17:15; Zab 31:6; Yer 10:8]

Hujitenga na rehema zao wenyewe;

9Lakini mimi nitakutolea sadaka kwa sauti ya shukrani;[#Zab 50:14; 66:13-15; Hos 14:2; Ebr 13:15]

Nitaziondoa nadhiri zangu.

Wokovu hutoka kwa BWANA.

10BWANA akasema na yule samaki, naye akamtapika Yona pwani.[#Yon 1:17; Mt 8:9]

Swahili Union Version (SUV): © Bible Society of Tanzania and Bible Society of Kenya, 1952, 1997. All rights reserved. lt/pgt ltpgtSwahili Union Version (SUV): Hakimiliki -1952, 1997: kwa: Chama cha Biblia cha Tanzania na Chama cha Biblia cha Kenya. Haki zote zimehifadhiwa.
Published by: Bible Society of Tanzania