The chat will start when you send the first message.
1BWANA, ni nani atakayekaa[#Zab 2:5]
Katika hema yako?
Ni nani atakayefanya maskani yake
Katika kilima chako kitakatifu?
2Ni mtu aendaye kwa ukamilifu,[#Zab 84:11; Isa 33:15,16]
Na kutenda haki.
Asemaye kweli kwa moyo wake,
3Asiyesingizia kwa ulimi wake.
Wala hakumtenda mwenziwe mabaya,
Wala hakumsengenya jirani yake.
4Machoni pake mtu asiyefaa hudharauliwa,[#Yos 9:18-20]
Bali huwaheshimu wamchao BWANA
Ingawa ameapa kwa hasara yake,
Hayabadili maneno yake.
5Hakutoa fedha yake apate kula riba,[#Eze 18:8,9]
Hakutwaa rushwa amwangamize asiye na hatia.
Mtu atendaye mambo hayo
Hataondoshwa milele.