The chat will start when you send the first message.
1BWANA ametamalaki, mataifa wanatetemeka;[#Kut 25:22]
Ameketi juu ya makerubi, nchi inatikisika.
2BWANA katika Sayuni ni mkuu,
Naye ametukuka juu ya mataifa yote.
3Na walishukuru jina lake kuu la kuhofiwa;[#Kum 28:58; Isa 6:3; Ufu 4:8]
Ndiye mtakatifu.
4Nguvu za mfalme nazo zapenda hukumu;[#Kum 32:3,4; Ayu 36:5; Isa 11:3-5; Yer 23:5; Mwa 18:25]
Wewe ndiwe uliyeithibitisha adili;
Ulifanya hukumu na haki katika Yakobo.
5Mtukuzeni BWANA, Mungu wetu;[#1 Nya 28:2; Zab 132:7; Isa 66:1]
Sujuduni penye kiti cha miguu yake;
Ndiye mtakatifu.
6Musa na Haruni miongoni mwa makuhani wake,
Na Samweli miongoni mwao waliitiao jina lake,
Walipomwita Bwana aliwaitikia;
7Katika nguzo ya wingu alikuwa akisema nao.[#Kut 19:9; Kut 33:9; Hes 12:5]
Walishika shuhuda zake na amri aliyowapa.
8Ee BWANA, Mungu wetu, ndiwe uliyewajibu;[#Hes 14:20; Sef 3:7; Kum 9:20]
Ulikuwa kwao Mungu mwenye kusamehe
Ingawa uliwapatiliza matendo yao.
9Mtukuzeni BWANA, Mungu wetu;
Sujuduni mkiukabili mlima wake mtakatifu;
Maana BWANA, Mungu wetu, ndiye mtakatifu.