The chat will start when you send the first message.
1NAMI nilipokuja kwenu ndugu, sikuja niwakhubiri siri ya Mungu kwa ufasaha wa maneno, wala kwa hekima.
2Maana naliazimu nisijue neno kwenu illa Yesu Kristo, nae amesulibiwa.
3Nami nalikuwako kwenu katika hali ya udhaifu na khofu na matetemeko mengi.
4Na neno langu na kukhubiri kwangu hakukuwa kwa maneno ya hekima ya kibinadamu yenye kushawishi akili za watu, bali kwa dalili za Roho zenye nguvu,
5imani yenu isiwe katika hekima ya wana Adamu, bali katika nguvu za Mungu.
6Illakini iko hekima tusemayo kati ya wakamilifu; nayo si hekima ya dunia hii, wala yao wanaoitawala dunia hii, wanaobatilishwa;
7bali twanena hekima ya Mungu katika fumbo, ile iliyofichwa, ambayo Mungu aliiazimu tangu asili, kwa utukufu wetu;
8ambayo wenye kutawala dunia hii hawakuijua hatta mmoja; maana kama wangaliijua, wasingalimsulibisha Bwana wa utukufu;
9lakini, kama ilivyoandikwa,
Mambo ambayo jicho halikuyaona wala sikio halikuyasikia,
Wala hayakuingia katika moyo wa kibinadamu,
Mambo ambayo Mungu aliwaandalia wampendao.
10Lakini Mungu ametufunulia sisi kwa Roho yake. Maana Roho huchunguza yote, hatta mafumbo ya Mungu.
11Maana ni nani ayajuae mambo ya bin Adamu illa roho ya bin Adamu iliyo ndani yake? Na vivyo hivyo mambo ya Mungu hakuna ayajuae illa Roho ya Mungu.
12Na sisi hatukuipokea roho ya dunia, bali Roho itokayo kwa Mungu, tupate kuyajua tuliyokarimiwa na Mungu.
13Nayo twayanena, si kwa maneno tuliyofundishwa na hekima ya binadamu, bali tuliyofimdishwa na Roho, tukiyalinganisha mamho ya rohoni na mambo va rohoni.
14Bassi mwana Adamu wa tabia ya asili hayapokei mambo ya Mungu; maana kwake huyu ni mapumbavu, wala hawezi kuyajua, kwa kuwa yatambulikana kwa jinsi ya rohoni.
15Lakini mtu wa rohoni huvatambua yote, wala yeye hatambuliwi na mtu.
16Maana ni nani aliyejua nia ya Bwana, amwelemishe? Lakini sisi tuna nia ya Kristo.