The chat will start when you send the first message.
1LAKINI nafsini mwangu nalikusudia hivi, nisije kwenu tena kwa huzuni.
2Maana mimi nikiwatia huzuni, hassi ni nani anifurahishae illa yeye ahuzunishwae nami?
3Nami naliwaandikia neno lili hili, illi, nijapo nisitiwe huzuni na wale ambao ilinipasa kuwafurahia; nikiwatumainia ninyi nyote kwamba furaha yangu ni yenu nyote pia.
4Maana katika shidda nyingi na dhiiki ya moyo niliwaandikieni nikitoka machozi mengi; si kwamba mhuzunishwe, bali mpate kujua upendo wangu nilio nao kwenu jinsi ulivyo mwingi.
5Lakini iwapo mtu amehuzunisha, hakunihuzunisha mimi, bali kwa sehemu ninyi nyote, nisije nikawalemea.
6Yamtosha mtu wa jinsi hii adhabu ile aliyopewa na walio wengi;
7hatta, kiuyume cha hiyo, ni afadhali mmsamehe na kumfariji, mtu kama huyu asije akatoswa katika huzuni ipitayo kiasi.
8Kwa hiyo nawasihi kumthubutishia upendo wenu.
9Maana naliandika kwa sababu hii pia, illi nipate bayana kwenu kwamba m wenye kutii katika mambo yote.
10Maana kama mkimsamehe mtu lo lote, na mimi; kwa maana mimi nami, ikiwa nimemsamehe mtu neno lo lote, nimemsamehe kwa ajili yenu mbele ya Kristo,
11Shetani asije akapata kutushinda; kwa maana sisi si wajinga, tunajua fikara zake.
12Bassi nilipofika Troa kwa ajili ya Injili ya Kristo nikafunguliwa mlango katika Bwana,
13sikupata raha nafsini mwangu, kwa sababu sikumwona Tito ndugu yangu, bali niliagana nao, nikaondoka kwenda Makedonia.
14Mungu ashukuriwe, anaetushangiliza daima katika Kristo, na kuyadhihirisha manukato ya hawa wamjuao killa pahali kwa kazi yetu.
15Kwa maana sisi tu manukato va Kristo, mbele za Mungu, katika wao wanaookolewa, na katika wao wanaopotea;
16katika hao wa kwanza manukato ya mauti yao waendao hatta mauti; katika hao wengine manukato ya uzima wao waendao hatta uzima. Na nani atoshae kwa mambo haya?
17Kwa maana sisi si kama wengi, walighoshio neno la Mungu; bali kama watu wasemao kwa weupe wa moyo, kaina watu watumwao na Mungu, mbele za Mungu, twanena katika Kristo.