Matendo 17

Matendo 17

1WAKIISHA kupita kati ya Amfipoli na Apollonia wakafika Thessalonika, na hapo palikuwa na sunagogi la Wayahudi.

2Na Paolo, kama ilivyokuwa desturi yake, akaingia mle walimo, akahujiana nao kwa maneno yii maandiko sabato tatu,

3akiyafunua na kuwaeleza ya kwamba ilimpasa Kristo kuteswa, na kufufuka katika wafu; na ya kama, Yesu huyu ninaewapasha ninyi khabari zake ndiye Kristo.

4Wengine wakaamini, wakasuhubiana na Paolo na Sila; na Wayunani waliomcha Mungu, wengi sana, na wanawake wenye eheo si wachache.

5Na Wayahudi wasioamini wakaona wivu, wakajitwalia watu kadha wa kadha katika watu ovyo wasio na sifa njema wakakutanisha mkutano, wakafanya ghasia mjini, wakawaendea watu wa nyumba ya Yason wakataka kuwapeleka mbele ya watu wa mji;

6na wasipowakuta, wakamkokota Yason na baadhi ya ndugu mbele ya wakubwa wa mji, wakipiga kelele, wakisema, Watu hawa walioupindua ulimwengu wamefika na huku,

7Yason akawakaribisha; na hawa wote wanatenda mambo yaliyo kinyume cha amri za Kaisari, wakisema ya kwamba yupo mfalme mwingine, aitwae Yesu.

8Wakautabarakisha nle mkutano na wakubwa wa mji walipoyasikia hayo.

9Nao walipokwisha kumtoza dhamana Yason na wenziwe wakawaacha waende zao.

10Marra ndugu wakawapeleka Paolo na Sila usiku hatta Beroya. Walipofika huko wakaingia katika sunagogi la Wayahudi.

11Watu hawa walikuwa waungwana kuliko wale wa Thessaloniki, kwa kuwa walilipokea Neno kwa uelekefu wa moyo, wakayachunguza maandiko, waone kwamba mambo hayo ndivyo yalivyo.

12Wafu wengi wakaamini miongoni mwao, nao wanawake wa Kiyunani wenye cheo, na wanaume si wachache.

13Lakini Wayahudi wa Thessaloniki walipopata khabari ya kwamba Neno la Mungu linakhubiriwa na Paolo katika Beroya, wakaenda huko wakawachafua makutano.

14Marra hiyo wale ndugu wakampeleka Paolo aende zake kana kwamba anakwenda njia ya pwani; bali Sila na Timotheo wakashinda huko.

15Nao walimsindikiza Paolo wakampeleka hatta Athene; na wakiisha kupokea maagizo kuwapelekea Sila na Timotheo, ya kama wasikawie kumfuata, wakaenda zao.

16Paolo alipokuwa akiwangojea katika Athene akaona jinsi mji ule ulivyojaa sanamu, roho yake ilichukizwa sana ndani yake.

17Bassi katika sunagogi akahujiana na Wayahudi nao waliomcha Mungu, na killa siku sokoni na wale waliokutana nae.

18Na baadhi ya Waepikurio na Wastoiko, matilosofo, wakakutana nae. Wengine wakasema, Mtu huyu mwenye maneno mengi anataka kusema nini? Wengine walisema, Anaonekana kuwa mtangaza khabari za miungu migeni, kwa maana alikuwa akikhubiri khabari za Yesu na ufufuo.

19Wakamshika, wakamchukua hatta Areopago, wakisema, Je, twaweza kujua maana ya elimu hii mpya inenwayo nawe?

20Kwa maana unaleta mambo mageni masikioni mwetu, tutapenda kujua, bassi, maana ya mambo haya.

21Kwa maana Waathene na wageni waliokaa huko walikuwa hawana faragha kwa neno lo lote illa kutoa khabari na kusikiliza khabari za jambo jipya.

22Paolo akasimaina katikati ya Areopago, tikasema,

Enyi watu wa Athene, katika mambo yote naona ya kuwa ninyi ni watu wa kutafakari sana mambo ya dini.

23Kwa sababu nilipokuwa nikipita huko na huko na kuyaona maabudu yenu, naliona madhliahu iliyoandikwa maneno haya, Kwa Mungu yule asiyejulikana. Bassi mimi nawakhubirini khabari zake yeye ambae ninyi mnamwabudu hila kumjua.

24Mungu aliyeufanya ulimwengu na vitu vyote vilivyomo, yeye, kwa kuwa ni Bwana wa mbingu na inchi, hakai katika hekalu zilizojengwa kwa mikono:

25wala hatumikiwi kwa mikono ya wana Adamu kana kwamba anahitaji kitu cho chote; kwa maana ndiye anaewapa wote uzima na pumzi na vitu vyote.

26Nae alifanya killa taifa ya wana Adamu kuwa wa damu moja, wakae juu ya uso wa inchi yote, akiisha kuwaandikia nyakati alizowaamuru tangu zamani, na mipaka ya makazi yao;

27illi wamtafute Mungu, ingawa ni kwa kupapasapapasa, wakamwone, ijapokuwa hawi mbali na killa mmoja wenu.

28Kwa maana ndani yake tunaishi, tunakwenda, tuna uhayi wetu. Kama vile mmoja wenu, mtunga mashairi, alivyosema, Maana sisi sote tu wazao wake.

29Bassi, kwa kuwa sisi tu wazao wa Mungu, haitupasi kudhani ya kuwa Uungu ni mfano wa dhahabu au fedha au jiwe, vitu vilivyochongwa kwa ustadi na akili za wana Adamu.

30Bassi zamani zile za ujinga Mungu alijifanya kama hauoni; bali sasa anawakhuhiri watu wote wa killa mahali watubu.

31Kwa maana ameweka siku atakayowahukumu walimwengu kwa haki, kwa ujumbe wa mtu yule aliyemchagua; nae amewapa watu wote bayana ya mambo haya kwa kumfufua katika wafu.

32Bassi waliposikia khabari za ufufuo wa wafu wengine wakadhihaki: wengine wakasema, Tutakusikiliza tena khabari hiyo.

33Bassi Paolo akaondoka akawaacha.

34Baadhi ya wanaume wakashikamana nae, wakaamini; katika hao alikuwamo Dionuso, Mwareopago, na mwanamke mmoja jina lake Damari, na watu wengine pamoja na hao.

Swahili New Testament © Bible Society of Tanzania, 1921.
Published by: Bible Society of Tanzania