The chat will start when you send the first message.
1NA ninyi, mlipokmva wafu kwa sababu ya makosa yenu na dhambi zemi,
2mlizoziendea zamani kwa kuifuata kawaida ya ulimwengu huu, na kwa kumfuata mfalme wa uwezo wa anga, roho yule atendae kazi sasa katika wana wa kuasi;
3ambazo sisi nasi sote tuliziendea, hapo zamani, katika tamaa za mwili wetu, tukiyatimiza mapenzi ya mwili wetu na ya nia zetu, tukawa kwa tabia yetu watoto wa ghadhabu kama na hao wengine.
4Lakini Mungu kwa kuwa mwingi wa rehema, kwa mapenzi yake makuu aliyotupenda,
5hatta wakati ule tulipokuwa wafu kwa sababu ya makosa yetu, alituhuisha pamoja na Kristo (mmeokolewa kwa neema);
6akatufufua pamoja nae, akatuketisha pamoja nae katika ulimwengu wa roho katika Kristo Yesu:
7illi katika zamani zinazokuja audhihirishe wingi wa neema yake upitao kiasi kwa wema wake kwetu katika Kristo Yesu.
8Maana mmeokolewa kwa neema, kwa njia ya imani; na hiyo haikutokana na nafsi zenu, ni kipawa cha Mungu:
9wala si kwa matendo, asije mtu awae yote akajisifu.
10Maana tu kazi yake, tuliumbwa katika Kristo Yesu, tutende matendo mema, ambayo Mungu aliyatengeneza tokea awali illi tuenende nayo.
11Kwa ajili ya hayo kumbukeni kwamba zamani, ninyi mlio watu wa mataifa kwa jinsi ya mwili, mnaoitwa jina lenu wasiotahiriwra na wale wanaoitwa jina lao waliotahiriwa, yaani tohara ya mwili kwa mikono:
12kwamba zamani zile mlikuwa hamna Kristo, mmefarakana na jamii ya Israeli, wageni, wasio wa maagano ya ahadi; mlikuwa hamna tumaini, hamna Mungu duniani.
13Lakini sasa, katika Kristo Yesu, ninyi mliokuwa mbali hapo kwanza, mmekuwa karibu kwa damu ya Kristo.
14Maana yeye ndiye amani yetu, aliyetufanya sisi sote tuliokuwa wawili kuwa mmoja, akakibomoa kiyambaza cha kati kilichotutenga,
15akiisha kuuondoa kwa mwili wake ule uadui, ndio sharia ya amri zilizo katika maagizo; illi afanye wawili kuwa mtu mpya mmoja ndani ya nafsi yake, akifanya amani;
16na kuwapatanisha wote wawili na Mungu katika mwili mmoja, kwa msalaba, akiisha kuuua ule uadui kwa huo msalaba;
17akaja, akakhubiri amani kwenu ninyi mliokuwa mbali, na kwao waliokuwa karibu.
18Maana kwa yeye sisi sote tumepata njia ya kumkaribia Mungu Baba katika Roho mmoja.
19Bassi tangu sasa ninyi si wapitaji wala wageni, bali ninyi ni wenyeji pamoja na watakatifu, watu wa nyumba ya Mungu,
20mmejengwa juu ya misingi ya mitume na manabii, na Kristo Yesu mwenyewe ni jiwe kuu la pembeni;
21katika yeye jengo lote likiungamanishwa vema linakua hatta liwe hekalu takatifu katika Bwana;
22katika yeye na ninyi mnajengwa pamoja kuwa maskani ya Mungu katika Roho.