Waefeso 4

Waefeso 4

1BASSI nawasihini, mimi niliye mfungwa katika Bwana, mwenende kama inavyoustahili wito wenu mlioitiwa,

2kwa unyenyekevu wote na upole, kwa uvumilivu, mkichukuliana katika upendano;

3mkijitahidi kuuhifadhi umoja wa Roho katika kifungo cha amani.

4Mwili mmoja, na Roho moja, kama na mlivyoitwa katika tumaini moja la wito wenu;

5Bwana mmoja, imani moja, ubatizo umoja,

6Mungu mmoja, nae Baba wa wote, aliye juu yote, na kwa yote, na katika yote.

7Lakini killa mmoja wetu alipewa neema, kwa kadiri ya kipawa cha Kristo.

8Kwa biyo asema,

Alipopanda juu, aliteka mateka,

Akawapa watu vipawa.

9(Bassi, neno lile, Alipanda, maana yake nini kania sio kusema kwamba alishuka hatta pande za chini za inchi?

10Aliyeshuka ndiye aliyepanda juu sana kupita mbingu zote, vitu vyote vijae nae.)

11Na yeye aliwatoa wengine kuwa mitume; na wengine kuwa manabii; na wengine kuwa wainjilisti, na wengine kuwa wachungaji, na waalimu,

12kwa kusudi la kuwakamilisha watakatifu, kazi ya khuduma itendeke, mwili wa Kristo ujengwe;

13hatta wote tutakapoufikia umoja wa imani, na kumfahamu sana Mwana wa Mungu, tuwe watu wakamilifu, hatta cheo cha kimo cha utimilifu wa Kristo;

14illi tusiwe tena watoto wachanga, tukitupwa huku na huku, na kuchukulivva kwa killa upepo wa elimu, kwa bila ya watu, kwa ujanja, tukifuata njia za udanganyifu;

15lakini tukiishika kweli katika upendo, tukue mpaka tumfikie ycye katika yote, aliye kichwa, Kristo;

16katika yeye mwili wote ukiungamanishwa na kushikanishwa, kwa msaada wa killa kiungo, kwa kadiri ya kazi ya killa sehemu moja moja, huukuza mwili upate kujijenga wenyewe katika upendo.

17Bassi nasema neno bili, tena nashuhudu katika Bwana, tangu sasa msienende kama Mataifa waendavyo, katika ubatili wa nia zao,

18akili zao zimetiwa giza, wamekaa mbali na uzima wa Mungu, kwa sababu ya ujinga uliomo niwao, kwa sababu mioyo yao imekufa ganzi:

19watu waliopooza kabisa, wamejitia katika mambo ya ufasiki, wapate kufanyiza killa namna ya uchafu kwa kutamani.

20Bali ninyi hamkujifunza hivi khabari za Kristo;

21mkiwa mwalimsikia mkafundishwa katika yeye, kama ilivyo kweli katika Yesu;

22mvue kwa khabari ya desturi za kwanza mtu wa zamani, anaeharibiwa kwa kuzifuata tamaa zenye kudanganya;

23na mfanywe wapya kwa roho ya nia zenu,

24mkavae mtu mpya, aliyeumbwa kwa namna ya Mungu katika baki na utakatifu wa kweli.

25Bassi uvueni uwongo, mkaseme kweli killa mtu na jirani yake; kwa maana tu viungo, killa mmoja kiungo cha wenzake.

26Mwe na ghadhabu, wala msifanye dhambi; jua lisichiwe na uchugu wenu bado kukutokeni;

27wala msimpe nafasi Shetani.

28Mwibaji asiibe tena; bali afadhali afanye juhudi, akitenda kazi iliyo njema kwa mikono yake mwenyewe, apafe kuwa na kitu cha kumgawia mhitaji.

29Neno lo lote lililo ovu lisitoke vinywani mwenu, bali lililo jema la kumfaa mwenye kuhitaji, liwape neema wanaosikia.

30Wala msimhuzunishe Roho yule Mtakatifu wa Mungu; kwa yeye mlitiwa muhuri mpaka siku ya ukombozi.

31Uchungu wote na hasira na ghadhabu na kelele na matukano yaondoke kwenu, pamoja na killa ubaya;

32tena mwe wafadhili ninyi kwa ninyi, wenye huruma, mkiachiliana, kama na Mungu katika Kristo alivyowaachilia ninyi.

Swahili New Testament © Bible Society of Tanzania, 1921.
Published by: Bible Society of Tanzania