The chat will start when you send the first message.
1BASSI mwe wafuasi wa Mungu, kama watoto wanaopendwa;
2mkaenende katika upendo, kama na Kristo alivyowapenda ninyi, akajitoa kwa ajili yetu, sadaka na dhabihu kwa Mungu, kuwa harufu nzuri.
3Lakini uasharati na uchafu wote au kutamani kusinenwe kwenu kabisa, kama iwastahilivyo watakatifu;
4wala aibu wala maneno ya upuuzi wala ubishi; haya hayapendezi; bali afadhali kushukuru.
5Maana neno hili mnalijua kwa kulifaliamu, kwamba hapana asharati, wala mchafu, wala mtu wa tamaa, ndiye mwabudu sanamu, aliye na urithi katika ufalme wa Kristo na Mungu.
6Mtu asiwadanganye kwa maneno yasiyo maana; maana kwa sababu ya haya ghadhabu ya Mungu huwajia wana wa uasi.
7Bassi msishirikiane nao.
8Kwa maana zamani mlikuwa giza, bali sasa nuru katika Bwana; enendeni kama watoto wa nuru;
9(kwa kuwa tunda la nura ni katika wema wote na haki na kweli);
10mkihakiki nini impendezayo Bwana.
11Wala msishirikiane na matendo yasiyozaa ya giza, bali myakemee;
12kwa kuwa yanayotendeka nao kwa siri, ni aibu hatta kuyanena.
13Lakini yote yakemewapo, hudhihirishwa na nuru; maana killa kitu kinachodhihirisha ni nuru.
14Kwa biyo anena, Amka, wewe usinziae, kafufuka, na Kristo atakuangaza.
15Angalieni sana, bassi, jinsi mnavyoenenda, si kama watu wasio hekima, bali kama wenye hekima;
16mkiukomboa wakati, kwa maana zamani bizi zina novu.
17Kwa sababu hii msiwe wajinga, bali watu wanaofahamu nini mapenzi ya Bwana.
18Tena msilevye kwa mvinyo, kwa kuwa haina kiasi, bali mjazwe Roho;
19mkisemezana kwa zaburi na fenzi na nyimbo za roho, mkiimba na kumshangilia Bwana mioyoni mwenu;
20mkimshukuru Mungu Baba siku zote kwa mambo yote, katika jina lake Bwana wetu Yesu Kristo;
21mkitumikiana katika khofu ya Kristo.
22Ninyi wake, watumikieni waume zenu kama kumtumikia Bwana wetu.
23Maana mume ni kichwa cha mke, kama nae Kristo ni kichwa cha kanisa; nae ni mwokozi wa mwili.
24Kwa hivyo kama Kanisa limtumikiavyo Kristo, vivyo hivyo nao wake wawatumikie waume zao katika killa jambo.
25Ninyi waume, wapendeni wake zenu, kama Kristo alivyolipenda Kanisa, akajitoa kwa ajili yake,
26kusudi alitakase na kulisafisha kwa maji, na kwa Neno;
27apate kujiletea Kanisa tukufu lisilo na ila ama kunyanzi ama lo lole kama haya; bali liwe takatifu na lisilo na mawaa.
28Vivyo hivyo imewapasa waume kuwapenda wake zao kama miili yao wenyewe. Ampendae mkewe hujipenda nafsi yake;
29maana hakuna mtu anaechukia mwili wtike, bali huulisha na kuutunza, kama Bwana anavyolitendea Kanisa;
30kwa kuwa tu viungo vya mwili wake, na nyama yake, na mifupa yake.
31Kwa sababu hiyo mtu atamwacha haha yake na mama yake, ataamhatana na mkewe; nao wawili watakuwa mwili mmoja.
32Hii ni siri kubwa; lakini nanena khabari ya Kristo na Kanisa.
33Illakini killa mtu ampende mke wake kama nafsi yake mwenyewe; na mke asikose kumstahi mumewe.