Waebrania 4

Waebrania 4

1BASSI, ikiwa ikaliko abadi ya kuingia katika raha yake, na tuogope, mmoja wenu asije akaonekana ameikosa.

2Maana ni kweli, sisi nasi tumekhubiriwa khabari njema kama hao. Lakini neno lile lililosikiwa halikuwafaa bao, kwa sababu halikuchanganyika na imani ndani yao waliosikia.

3Maana sisi tulioamini tunaingia katika raba ile; kama vile alivyonena,

Nilivyoapa kwa hasira yangu,

Hawataingia katika raha yangu:

ijapokuwa zile kazi zilimalizika tangu kuwekwa misingi ya ulimwengu.

4Kwa maana amenena siku ya saba niabali fullani hivi, Mungu alistarche siku ya saba, akaziacha kazi zake zote;

5na hapa napo, Hawataingia katika raha yangu.

6Bassi, kwa kuwa neno hili limebaki kwamba wako watu watakaoingia, na wale waliokhubiriwa khabari ile zamani walikosa kuingia kwa sababu ya kuasi kwao,

7aweka tena siku fullani, akisema katika Daud baada ya muda mwingi namna hii, Leo; kama ilivyonenwa tangu zamani, Leo kama mtasikia sauti yake, msiifanye migumu mioyo yenu.

8Maana kama Yoshua angaliwapa raha, asingaliinena siku nyingine baadae.

9Bassi, imesalia hali ya raha kwa watu wa Mungu.

10Kwa maana yeye aliyeingia katika raha yake amestarche mwenyewe baada ya kazi yake, kama vile Mungu alivyostarche baada ya kazi zake.

11Bassi, na tufanye bidii kuingia katika raha ile, mtu ye yote asije akaanguka kwti mfano huo huo wa kuasi.

12Maana Neno la Mungu li hayi, tena lina nguvu, tena lina ukali kuliko ukali wa upanga ukatao kuwili, tena lachoma kiasi cha kuzigawanya nafsi na roho, na viungo na mafuta yaliyomo ndani yake; li jepesi kuyatambua mawazo na makusudi ya moyo.

13Wala hakuna kiumbe kisicho wazi mbele zake, lakini vitu vyote vi utupu, na kufunuliwa machoni pake aliye na mambo yetu.

14Bassi, iwapo tunae kuhani mkuu aliyeingia katika mbingu, Yesu, Mwana wa Mungu, tujashike sana maungamo yetu.

15Kwa kuwa hatuna kuhani mkuu asiyeweza kuyachukua mambo yetu ya udhaifu; bali yeye alijuribiwa sawa sawa na sisi katika mambo yote, bila dhambi.

16Bassi na tukikaribie kiti cha neema kwa nthubuitifu, illi tupewe rehema, na kupata neema ya kutusaidia wakati wa mahitaji.

Swahili New Testament © Bible Society of Tanzania, 1921.
Published by: Bible Society of Tanzania