Waebrania 7

Waebrania 7

1KWA maana Meikizedeki huyo, mfalme wa Salemi, kuhani wa Mungu aliye juu, aliyekutana na Ibrahimu baada ya kuwapiga wafalme, alimbariki;

2aliyegawiwa na Ibrahimu sehemu ya kumi ya vitu vyote; (kwanza kwa tafsiri, mfalme wa haki, tena, mfalme wa Salemi, maana yake, mfalme wa amani;

3hana baba, hana mama, hana wazazi, hana mwanzo wa siku zake, wala mwisho wa uhayi wake, bali amefanauishwa na Mwaua wa Mungu,) adumu kuhani milele.

4Bassi, angalieni jinsi mtu huyo alivyokuwa mkuu, ambae Ibrahimu, baba yetu mkuu, alimpa sehemu ya kumi ya maleka yaliyo mema.

5Na katika wana wa Lawi, wale waupatao ukuhani, wana amri kutwaa sehemu ya kumi kwa watu wao, yaani ndugu zao, kwa agizo la sharia, ijapokuwa wametoka katika viuno vya Ibrahimu.

6Bali yeye, ambae uzazi wake haukuhesabiwa kuwa umetoka kwa hao, alitwaa sehemu ya kumi kwa Ibrahimu, akambariki yeye aliye na ile ahadi.

7Na haikanushiki kwamba mdogo hubarikiwa na mkubwa.

8Na hapo wana Adamu wapaswao na kufa hutwaa sehemu ya kumi; bali huku yeye ashubudiwae kwamba yu hayi.

9Na yaweza kusemwa ya kuwa, kwa njia ya Ibrahimu, hatta Lawi apokeae sehemu ya kumi alitoa sehemu ya kumi;

10kwa maana alikuwa katika viuno vya bada yake Ibrahimu, hapo Melkizedeki alipokutana nae.

11Bassi, kama ukamilifu ulikuwapo kwa ukuhani wa Lawi: (maana watu wale waliipata sharia kwa huo) kulikuwa na haja gani tena kuhani mwingine aondoke, wa daraja la Melkizedeki, wala si kwa daraja la Haruni?

12Maana ukuhani ule ukihadilika, hapana buddi sharia nayo ibadilike.

13Maana yeye aliyenenwa hayo alikuwa mshirika wa kahila nyingine, wala hapana mtu wa kahila hii aliyeikhudumia madhbahu.

14Maana ni dhahiri kwamba Bwana wetu alitoka katika Yuda, kabila ambayo Musa hakunena neno lolote la kuikhusu katika mambo ya ukuhani.

15Tena hayo tusemayo ni dhahiri sana zaidi, ikiwa ametokea kuhani mwingine kwa mfano wa Melkizedeki;

16asiyekuwa kuhani kwa sharia ya amri iliyo ya jinsi ya mwili, bali kwa nguvu za uzima usio na kikomo:

17maana ashuhudu, kwamba, Wewe u kuliani hatta milele kwa daraja la Melkizedeki.

18Maana, kima kubatiliwa kwa ile amri iliyotangulia, kwa sababu ya udhaifu wake, na kutokufaa kwake

19(kwa maana sharia ile haikukamilisha neno); na pamoja na haya kuliingizwa matumaini yaliyo mazuri zaidi, ambayo kwayo twamkaribia Mungu.

20Na kwa kuwa haikuwa pasipo kiapo,

21(maana wale walifanywa makuhani pasipo kiapo; hali yeye, pamoja na kiapo, kwa yeye aliyemwambia, Bwana ameapa wala hataghairi, Wewe kuhani hatta milele kwa daraja la Melkizedeki;)

22bassi kwa kadiri hii Yesu amekuwa mdhamini wa agano lililo hora zaidi.

23Tena wale walifanywa makuhani wengi, kwa sababu wazuiliwa na manti wasikae;

24hali yeye, kwa kuwa akaa milele, ana ukuhani usioondoka.

25Nae, kwa sababu hii, aweza kuwaokoa kabisa wao wajao kwa Mungu kwa yeye; maana yu hayi siku zote illi awaombee.

26Maana ilipendeza sisi tuwe na kuhani mkuu wa namna hii, aliye mtakatifu, asiokuwa na uovu, asiokuua na waa lolote, aliyetengwa na wakosaji, aliyekuwa juu kuliko mbingu;

27asiye na baja killa siku, kwa mfano wa wale makuhani wakuu wengine, kwanza kutoa dhabihu kwa ajili ya dhambi zake mwenyewe, kiisha kwa ajili ya dhambi za watu; maana yeye alifanya hivi marra moja, alipojitoa nafsi yake.

28Maana torati yawaweka wana Adamu walio na unyonge kuwa makuhani wakuu; bali neno la kiapo kilichokuja baada ya torati limemweka Mwana, aliyekamilika hatta milele.

Swahili New Testament © Bible Society of Tanzania, 1921.
Published by: Bible Society of Tanzania