The chat will start when you send the first message.
1NIKAONA malaika akishuka kutoka mbinguni, mwenye ufunguo wa abuso, na mnyororo mkubwa mkononi mwake.
2Akamshika joka, yule nyoka wa zamani, aliye msingiziaji, Shetani, akamfunga miaka elfu,
3akamtupa katika abuso, akamfunga, akatia muhuri juu yake, asipate kuwadanganya mataifa tena, hatta ile miaka elfu itimie; na baada ya haya imepasa afunguliwe muaa mchache.
4Nikaona viti vya enzi, wakaketi juu yake, wakapewa hukumu: nikaona roho zao waliokatwa kichwa kwa ajili ya ushuhuda wa Yesu, na kwa ajili ya neno la Mungu, na hao wasiomsujudia nyama, wala sanamu yake, wala hawakuipokea alama yake katika vipaji vya nyuso zao, wala katika mikono yao; wakawa hayi, wakamiliki pamoja na Kristo miaka elfu.
5Na wafu waliosalia hawakuwa hayi, hatta ikatimia ile miaka elfu. Huo ndio ufufuo wa kwanza.
6Yu kheri, mtakatifu, aliye na sehemu katika ufufuo wa kwanza; juu ya hao mauti ya pili haina nguvu; bali watakuwa makuhani wa Mungu na wa Kristo, nao watamiliki pamoja nae miaka elfu.
7Na ile miaka elfu itakapokwisha, Shetani atafunguliwa atoke kifungoni mwake:
8nae atatoka kuwadanganya mataifa walio katika pembe nne za inchi, Gog na Magog, kuwakusanya kwa vita, ambao hesabu yao ni kama mchanga wa bahari.
9Wakapanda juu ya upana wa inchi, wakazinga kituo chta watakatifu, na mji uliopendwa. Moto ukashuka katika mbingu kutoka kwa Mungu, ukawala.
10Na yule Msingiziaji, mwenye kuwadanganya, akatupwa katika ziwa la moto na kiberiti, alimo yule nyama na yule nabii wa nwongo. Na wataumwa mchana na usiku hatta milele na milele.
11Nikaona kiti eba enzi, cheupe, kikubwa, nae aketiye juu yake; inchi na mbingu zikakimbia nso wake, na mahali pao hapakuonekana.
12Nikawaona wafu, wakubwa na wadogo, wamesimama mbele za Mungu; vitabu vikafunuliwa. Kitabu kingine kikafunuliwa, kilicho eha uzima, wafu wakahukumiwa kwa mambo ya matendo yao.
13Bahari ikawatoa wafu waliomo ndani yake. Mauti na Kuzimu zikawatoa wafu walio ndani yake. Wakahukumiwa killa mtu kwa kadiri ya matendo yao.
14Mauti na Kuzimu wakatupwa katika lile ziwa la moto. Hii ndio mauti ya pili.
15Na ikiwa mtu hakuonekana ameandikwa katika kitabu cha uzima, alitupwa katika lile ziwa la moto.